Wat. Fabiani, Papa na Sebastian, Mashahid
Kijani
Zaburi: Juma 2
SOMO 1: Ebr 8:6-13
Kuhani wetu sasa amepata huduma iliyo bora zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora. Maana kama lile la kwanza lingalikuwa halina upungufu, nafasi isingalitafutwa kwa lile la Pili. Maana, awalaumupo, asema, Angalia, siku zinakuja, asema Bwana, nami nitawatimizia nyumba ya Israelí na nyumba ya Yuda agano jipya; halitakuwa kama agano lile nililoagana na baba zao, katika situ ile nilipowashika mikono yao niwatoe katika nchi ya Misri. Kwa sababu hawakudumu katika agano langu, mimi nami sikuwajali, asema Bwana. Maana hili ndilo agano nitakaloagana na nyumba ya Israelí baada ya situ zile asema Bwana; nitawapa sheria zangu katika nia zao, na katika mikono yao nitaziandika; nami nitakuwa Mungu kwao, nao watakuwa vatu wangu. Nao hawatafundishana kila mtu na jirani yake, na kila mtu na ndugu yake, akisema, Mjue Bwana; kwa maana wote watanijua, tangu mdogo wao hata mkubwa wao. Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, sitazikumbuka tena. Kwa kule kusema, Agano jipía, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu na kuchakaa ki caribú na kutoweka.
WIMBO WA KATIKATI: Zab. 85:7, 9-13
- Ee Bwana, utuonyeshe rehema zako,
Utupe wokovu wako.
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu.
(K) Fadhili na kweli zimekutana. - Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na amani zimebusiana.
Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni. (K) - Naam, Bwana atatoa kilicho Chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zake kuwa njia. (K)
INJILI: Mk 3: 13-19
Yesu alipanda mlimani, akawaita aliowataka mwenyewe; wakamwendea. Akaweka watu kumi na wawili, wapate kuwa pamoja naye, na kwamba awatume kuhubiri, tena wawe na amri ya kutoa pepo. Akawaweka wale Thenashara; na Simoni akampa jina Petro; na Yakobo, mwana wa Zebedayo, na Yohane nduguye Yakobo, akawapa jina la Boanerge, maana yake, wana wa ngurumo; na Andrea, na filipo, na Bartholomayo, na Mathayo, na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Tadayo, na Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.
TAFAKARI:
SHERIA YA BWANA IMEANDIKWA ROHONI MWETU: Tunaona jinsi Agano la Kale liliwategemea Musa na manabii, wakiwa ndio waalimu wa hilo agano. Ila, Agano hili halikushughulikia dhambi kwa namna iliyofaa. Kinyume na hayo, Agano Jipya, linaondoa dhambi. Tunaalikwa kulitafakari Agano wenyewe na kulishiriki. Kanisa lipo kutoa mwongozo wa namna ya kuliishi Agano (Sheria ya Mungu) ambalo limeandikwa tayari rohoni na akilini mwetu. Kanisa linatufundisha tuutafute ushauri wa watu wafaao, tunapotaka kufanya maamuzi maalumu yahusuyo maisha yetu binafsi na jinsi ya kuishi na wenzetu. Siku zote usikilize moyo wako, kama kuna ambacho kinakusukuma kutenda jambo jema, nawe utapata amani. Ruhusu Sheria ya Mungu iutawale moyo wako ili uziepuke tamaa potovu. U mtoto wa Agano Jipya, Mungu amekuweka huru. Leo, Yesu anawateua mitume ili wawe naye na awatume wakauendeleze utume wake, na ili wote wamjue. Huu ni wajibu wako na wangu pia. Ni mwito wa kila Mkristo kuufanya utume, ili Ukristo uenee.