Aprili 16,2022; Jumamosi: Jumamosi Kuu

Masomo ya Mkesha wa Pasaka ambayo ni somo la Jumapili ya Pasaka: Gn 1: 1 — 2: 2 or 1: 1.26-31a/ Ps 104: 1-2. 5-6. 10. 12. 13-14. 24. 35 or Ps 33: 4-5. 6-7. 12-13. 20-22/ Gn 22: 1-18 or22: 1-2. 9a. 10-13. 15-18/ Ps 16: 5. 8. 9-10. 11/ Ex 14: 15 — 15: 1/ Ex 15: 1-2. 3-4. 5-6. 17-18/Is 54: 5-14/ Ps 30: 2. 4. 5-6. 11-12. 13/ Is 55: 1-11/ Is 12: 2-3. 4. 5-6/ Bar 3: 9-15. 32 — 4: 4/ Ps19: 8. 9. 10. 11/ Ez 36: 16-17a. 18-28/ Ps 42: 3. 5; 43: 3. 4 or Is 12: 2-3. 4bcd. 5-6 or Ps 51:12-13. 14-15. 18-19/ Rom 6: 3-11/ Ps 118: 1-2. 16-17. 22-23/ Lk 24: 1-12
Nyeupe
Zaburi: Tazama sala ya siku

Usiku Mtakatifu:

SOMO 1: Mwa 1: 1 — 2: 2 au 1: 1. 26-31a

(K) Nchi imejaa fadhili za Bwana. Zab: 33: 4-5. 6-7. 12-13. 20-22

SOMO 2: Mwa 22: 1-18 au 22: 1-2. 9a. 10-13. 15-18

Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia Wewe. Zab. 16:5, 8-11

SOMO 3: Kut 14: 15 — 15: 1
Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia Wewe. Zab. 16:5, 8-11

SOMO 4: Isa 54: 5-14

Ee Bwana nitakutukuza kwa maana umeniiua. Zab. 30:1,3-5, 10-12

SOMO 5: Isa 55:1-11

Ee Bwana nitakutukuza kwa maana umeniiua. Zab. 30:1,3-5, 10-12

SOMO 6: Bar 3: 9-15, 32 — 4: 4

Wewe unayo maneno ya uzima wa milele, Ee Bwana. Zab. 19:7-10 (K) Yh. 6:69

SOMO 7: Eze 36: 16-28

Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, ee Mungu. Zab. 42:2, 4; 43:3-4

SOMO 1: Rum 6: 3-11

Aleluya, Aleluya, Aleluya. Zab. 118:1-2, 16-17, 22-23

INJILI: Mt. 28:1-10

Hata sabato ilipokwisha, ikipambazuka siku ya kwanza ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Na tazama, palikuwa na tetemeko kubwa la nchi; kwa sababu malaika wa Bwana alishuka kutoka mbinguni, akaja akalivingirisha lile jiwe akalikalia. Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama theluji. Na kwa kumwogopa, wale walinzi wakatetemeka, wakawa kama wafu. Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, “Msiogope ninyi! Kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. Hayupo hapa; kwani amefufuka kama alivyosema! Njoni, mpatazame mahali alipolazwa. Nanyi nendeni upesi, mkawaambie wanafunzi wake, ‘Amefufuka katika wafu. Tazama, awatangulia kwenda Galilaya; ndiko mtakakomwona.’ Haya, nimekwisha waambia.” Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa hofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake habari. Na tazama, Yesu akakutana nao, akisema, “Salamu!” Wakakaribia wakamshika miguu, wakamsujudia. Kisha Yesu akawaambia, “Msiogope; enendeni, mkawaambie ndugu zangu waende Galilaya, ndiko watakakoniona.”

TAFAKARI
TUNAKUMBUSHWA TULIVYOTEKELEZEWA VIZURI MPANGO WA UKOMBOZI: Tumekombolewa kutoka dhambi na mauti. Si kwa maana kwamba hatutatenda tena dhambi, bali kwa maana tukitenda dhambi tunaweza kumwendea Mungu kwa Kitubio. Aidha si kwamba hatutakufa kibayolojia, la hasha! Tunachosema ni kuwa tukifa tukiwa ndani ya Yesu, tutafufuliwa katika kutoharibika mbinguni. Kwa namna hii, masomo na matendo katika ibada ya leo yanatukumbusha mambo Mungu aliyokusudia juu yetu. Tunamshukuru kwa kutufanyia yote mema, tumefunguliwa milango ya ukombozi. Tunawiwa deni la shukrani kwake kwani tulijilaza chini, Mungu akatuinua kwa masamaha na ukombozi. Tulijipoteza, Mungu akatutafuta hata kutupata na kutubeba mabegani mwake. Wanadamu kupitia kwa Adamu na Eva tulipotea, bali Mungu akaturejesha kwenye njia ya utukutu. Kwa kuwa tumepatikana, tujidumishe kwake kwa kutotenda dhambi. Kwa uaminifu tulipe deni letu kwa Mungu siku zote. Tutalipa hadi tuyapate matunda ya kazi ya ukombozi huu ndiyo kuiingia katika uzima wa milele, kukaa pamoja na Mungu na Mkombozi wetu. Mungu ametutayarishia na anatuitia pema, tusikatae kuingia pema.

SALA: Ee Mungu umetukumbusha usiku huu historia ya ukombozi wetu. Tumepata picha ya kazi kubwa ya uumbaji na ukombozi wetu. Tudumishe kwako na si kwa mwingine yeyote. Amina.