Novemba 30,2022; Jumatano: Juma La 1 La Majilio

Mt. Andrea, Mtume
Sikukuu
Nyekundu
Zaburi: Tazama sala ya siku
SOMO I: Rum. 10:9-18

Ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Kwa maana andiko lanena: Kila amwaminiye hatatahayaraki. Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; kwa kuwa: Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Basi wamwitaje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa: Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema: Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lakini nasema, je! wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.

Wimbo Wa Katikati: Zab. 19:1-4

 1. Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,
  Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
  Mchana husemezana na mchana,
  Usiku hutolea usiku maarifa.

(K) Sauti yao imeenea duniani mwote.

 1. Hakuna lugha wala maneno,
  Sauti yao haisikilikani.
  Sauti yao imeenea duniani mwote,
  Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu.(K)

INJILI: Mt. 4:18-22

Yesu alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi. Akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.” Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata; akaendelea mbele, akaona ndugu wangine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohane nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita. Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.

TAFAKARI
WALIACHA YOTE WAKAMFUATA: Kawaida kabisa anapoitwa mtu huuitika na kuzisikiliza sababu za mwito wenyewe. Petro na Andrea nduguye, Yakobo wa Zebedayo na Yohane nduguye waliposikia tu sauti ya Kristo inawaita walikuwa tayari kuacha vyote na kumfuata. Kristo anawaita ili wakae naye, wajifunze kwake na baadaye awatume kwenda kuuhubiri Ufalme wa Mungu. Imani chanzo chake ni kusikia na hawa mitume waliisikia hiyo sauti ya Kristo ikiwaita wakaacha yote walioyazoea wakamfuata. Ukristo umeenea sehemu mbalimbali za ulimwengu kwa Neno la Kristo lililoenezwa na mitume hao ambao walisikia sauti ya Kristo. Tumekuwa wafuasi kutokana na hawa mitume waliokuwa wafuasi wazuri. Wakristo wa siku hizi za leo pia tumeitwa kuwa wafuasi wazuri tukifuata mfano wa hao mitume waliokuwa tayari kueneza Injili. Nasi tukishaitafakari vema Injili ya Kristo tuiishi na tuipeleke kwa watu wengine.

SALA: Ee Bwana, neema yako iniwezeshe kuusikia vema mwito wako, nikae katika Neno lako niweze